
Baadhi ya wanafunzi bora wa kidato cha nne na sita, waliofanya vizuri katika masomo yao kwa mwaka 2010-2011, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, alipozungumza nao katika hafla ya kuwapongeza kutokana na kufaulu vizuri katika mitihani yao, huko Ikulu Mjini Zanzibar jana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipokea risala kutoka mwanafunzi Ali Omar Ali, kwa niaba ya wanafunzi bora wa kidato cha nne na sita, waliofanya vizuri katika masomo yao kwa mwaka 2010-2011, alipowapongeza ikulu Mjini Zanzibar jana.