Dk. Shein Apokea Waya wa Umeme Utakaopitishwa Baharini

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akisalimiana na Msaidizi Mtendaji Mkuu wa MCA-T kwa upande wa Zanzibar, Ahmed Rashid alipowasili Bandari ya Malindi Mjini Unguja kuupokea na kuukagua waya huo wa Umeme utakaolazwa kwa siku Kumi na mbili kutoka Ras-Kiromoni Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana na Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati, Ramadhan Abdalla Shaaban alipofika katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja Kuupokea na Kuukagua Waya wa Baharini utakaotumika katika Mradi wa Ulazaji waya wa pili wa Umeme kutoka Ras-Kiromoni Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar ukiwa katika Meli ya Kampuni ya Viscas kutoka nchini Japan. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akisalimiana na
Wahandisi wa Kampuni ya Viscas ya Ulazaji waya wa Umeme kutoka Nchini Japan alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja kuupokea na kuukagua waya huo wa Umeme utakaolazwa kwa siku Kumi na mbili kutoka Ras-Kiromoni Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]