Dk Shein aongoza mazishi ya Brig. Mwakanjuki

”] ”]

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, jana ameongoza mazishi ya marehemu Brigedia Jenerali mstaafu Adam Clement Mwakanjuki, yaliyofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.

Katika mazishi hayo, yaliyofanyika kwa taratibu zote za kijeshi ikiwa ni pamoja na kupigwa mizinga kumi na moja, viongozi mbali mbali wa siasa, Dini na Serikali, wananchi na wanafamilia walihudhuria katika mazishi hayo, ambapo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal nae alihudhuria.

Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania Abraham Shimbo, Wakuu wa vikosi vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na SMZ, Mawaziri, Wabunge na Wawakilishi walihudhuria. Mama Shadya Karume pia, alihudhuria. Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki alifariki dunia tarehe 19,4 mwaka huu.

Mwakanjuki alizaliwa Oktoba 17, 1939 katika Mtaa wa Kikwajuni, Wialaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar na hadi kifo cheke aliku ana umeri wa miaka 73.
”]
Akisoma risala fupi baada ya mazishi hayo, Katibu Mkuu, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Halid Salum Mohammed, alieleza kuwa marehemu alipata elimu yake ya msingi katika skuli iliyokuwa ikijulikana kwa jina la St Paul- Kiungani Zanzibar katika mwaka 1947 hadi 1954.

Vile vile mnamo mwaka 1955 hadi 1959, marehemu alipata fursa ya kujiunga na masomo ya sekondari katika Skuli ya St. Andrew ya Minaki, jijini Dar-es-Salaam ambapo kutokana na uhudari wake na umakini katika juhudi za kujitafutia elimu, marehemu alipata fursa ya kuendelea na masomo ya juu ya siasa katika Chuo Kikuu cha Fritz Hecket nchini Ujerumani Mashariki mnamo mwaka 1960 hadi 1962.

Baada ya mapinduzi ya mwaka 1964, marehemu alikuwa ni mmoja wa viongozi wa Umoja wa Wafanyakazi wa Zanzibar, na kuanzia mwaka 1964 hadi 1968 marehemu aliajiriwa na kufanyakazi katika Idara ya Mambo ya Nje ya Sererikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishikilia wadhifa wa Afisa Mambo ya Nje.

Marehemu alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) tarehe 24 Juni, 1969 akiwa na wadhifa wa Mwalimu wa siasa katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na baadae aliendelea na utumishi katika JWTZ katika nyadhifa mbali mbali.

Marehemu Mwakanjuki alifanikiwa kupandishwa Vyeo katika Ngazi tofauti ikiwa ni pamoja na Cheo cha Meja, Luteni Kanali, Cheo cha Kanali na hatimae mwaka 1988 alipandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali, Cheo ambacho aliendelea kwa nacho hadi alipostaafu jeshini tarehe 30.6.1994.

Miongoni mwa Medali alizowahi kutunukiwa ni Medali ya Uhuru, Medali ya Muungano, Medali ya Vita, Medali Kagera, Medali ya Miaka 20 ya JWTZ, Medali ya Utumishi Mrefu wa Tanzania na Medali ya Utumishi Uliotukuka Tanzania.

Kwa upande wa siasa Mwakanjuki alijiunga na Chama cHa Afro Shirazi (ASP) mwaka 1958, akiwa Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Minaki Aiodha katika mwaka 1958- 1959, alikuwa Kiongozi wa Chama Cha Wafanyakazi wa Kiafrika wa Zanzibar na kushiriki katika mikutano mbali mbali ya Chama pamoja na kushiriki kikamilifu katika harakati za Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12,1964.

Baada ya kuungana vyama vya ASP na TANU mwaka 1977 marehemu alijiunga na Chama Cha Mapinduzi kupitia Tawi la Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (MMJKT) liliopo Mkoa wa Dar-es-Salaam mnamo April 1977. Marehemu alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa tangu mwaka 1982 hadi alipofariki.

Marehemu Mwakanjuki alishika nyazifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikiwa ni pamoja na Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Waziri wa Kilimo, Mifugo, Mazingira na Ushirika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Katiba na Urawala Bora na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi.

Akitoa salamu za mkono wa pole za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa wafiwa na ndugu na jamaa wote Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud aliaeleza kuwa kifo hicho ni msiba mkubwa kwa wananchi wa Zanzibar na marehemu ataendelea kukumbukwa kwa ujasiri na utendahi wake wa kazi.

Nao wanafamilia walitoa shukurani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kusaidia mazishi hayo pamoja na kumsaid amarehemu tokea alipopata ajali mwaka 2007 hadi kufariki kwake sanajari na kutoa shukurani wa JWTZ kwa msaada wao mkubwa katika mazishi hayo. Marehemu ameacha kizuka mmoja na watoto saba.