Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho,(kushoto) Mshauri wa Rais Kilimo, Buruhani Saadat Haji,(kati) na Naibu Katibu Mkuu Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibar wanaoishi Nje ya Nchi, Saidi Natepe, wakiwa katika hafla ya kuapishwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiagana na Bw.Vuai Mwinyi Mohamed,baada ya kumuapisha leo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akitia saini hati ya kiapo baada ya kumuapisha Vuai Mwinyi Mohamed, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja, hafla ilifanyika leo, Ikulu Mjini Zanzibar. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Vuai Mwinyi Mohammed kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi Khamis.
Wengine waliohudhuria katika hafla hiyo ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib, Washauri wa Rais pamoja na viongozi wengine wa Serikali.