Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, (wa pili kushoto) akiagana na Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba jana baada ya Chakula cha Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni. {Pichana Ramadhan Othman, Ikulu.}
Baadhi ya Wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni Pemba jana {Picha na Ramadhan Othman, Ikulu}