Dk. Shein afanya mabadiliko Baraza la Mawaziri Zanzibar

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHESHIMIWA DKT. ALI MOHAMED SHEIN AMEFANYA MABADILIKO YA KUWABADILISHA WIZARA BAADHI YA MAWAZIRI KAMA IFUATAVYO:-

1. MHE. RAMADHAN ABDULLA SHAABAN – AMETEULIWA KUWA
WAZIRI WA ARDHI,
MAKAAZI MAJI NA NISHATI

2. MHE. ALI JUMA SHAMHUNA – AMETEULIWA KUWA
WAZIRI WA ELIMU NA
MAFUNZO YA AMALI.

3. MHE. SULEIMAN OTHMAN NYANGA – AMETEULIWA KUWA
WAZIRI WA KILIMO NA
MALIASILI.

4. MHE. MANSOOR YUSSUF HIMID – AMETEULIWA KUWA
MJUMBE WA BARAZA LA MAPINDUZI NA WAZIRI ASIEKUWA NA WIZARA MAALUM

5. MHE. ABDILLAH JIHAD HASSAN – AMETEULIWA KUWA
WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI

6. MHE. SAID ALI MBAROUK – AMETEULIWA KUWA
WAZIRI WA HABARI,
UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO

AIDHA, RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHESHIMIWA DKT. ALI MOHAMED SHEIN AMEMTEUA BW. SHEHA MOHAMMED SHEHA KUWA MSHAURI WA RAIS – PEMBA.

UTEUZI HUO UMEANZA LEO TAREHE 02 APRILI, 2012.

(DKT. ABDULHAMID Y. MZEE)
KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI
NA KATIBU MKUU KIONGOZI,
ZANZIBAR.

02 APRILI, 2012