Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, leo amefanya ziara ya kuwafariji wafiwa katika Mikoa mitatu ya Unguja kufuatia ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv. Spice Islander na kueleza kuwa serikali ina mpango wa kuijengea uwezo Idara ya Maafa ili kukabiliana na matukio na majanga mbali mbali hapa nchini.
Dk, Shein, alieleza hayo kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa akiwafariji wafiwa huko katika Mikoa mitatu ya Unguja ambapo asubuhi alianza na Wilaya ya Mjini huko katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani, Wilaya ya Magharibi ambapo wafiwa walikuwepo katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbweni, Kinduni kwa Kaskazini B, Chaani kwa Kaskazini A na Dunga kwa Wilaya ya Kati.
Katika ziara yake hiyo, Dk. Shein amefuatana na Mama Mwanamwema Shein pamoja na viongozi wengine mbali mbali wakiwemo Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Wawakilishi, Wakuu wa Mikoa husika pamoja na viongozi wa vyama vya siasa.
Dk. Shein alisema kuwa mbali ya kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Uchunguzi aliyoiunda na yale mapendekezo ya Baraza la Usalama pia, serikali imo katika mikakati ya kujiandaa kimazingira ili kuepuka ajali kama hiyo kutotokea tena.
Alisema kuwa kutokana na hali hilo ipo haja ya kuijengea uwezo Idara hiyo ya Maafa ambapo tayari washirika wengi wa maedneleo wameshaonesha nia ya kusaidia kuunga mkono juhudi za kuiimarisha Idara hiyo
Dk. Shein alisema kuwa Tume hiyo ya watu 10 aliyoiunda ikiongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Abdulhakim Ameir Issa pia, imejumuisha wataalamu kadhaa wa Sheria, manahodha waliobobea ambao wamefanya kazi kwa siku nyingi ndani na nje ya Tanzania, wahandisi wa bahari na wenye elimu ya vyombo vya bahari pamoja na wataalamu wengineo.
Aidha, Dk. Shein alisema kuwa mapendekezo yatakayotolewa na Tume hiyo yatafanyiwa kazi sambamba na yale yaliotolewa na Baraza la Usalama la Taifa ambapo pia, wananchi nao watapewa taarifa na kama kunahitajika hatua za kisheria basi zitachukuliwa.
Dk. Shein alieleza matumaini yake kuwa Tume hiyo itatoa taarifa kwa wakati muwafaka. Dk. Shein alisema kuwa serikali bado ina nia ya kununu meli nyengine kubwa ambayo itajumuisha safari kati ya Unguja na Pemba, na sehemu nyengine katika ukanda huu pale serikali itakapopata uwezo kwai ndio sababu kubwa inayokwanza kununuliwa meli mpya hiyo ni kutokana na bei za meli kuwa juu.
Alieleza kuwa kwa taarifa za uongozi wa juu wa Wizara ya Mawasiliano bei ya meli hivi sasa ni zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 40.
Mbali na hatua hiyo, Dk. Shein alisema kuwa kuongezeka kwa watu hapa Zanzibar ikilinganishwa na sense baa day a Mapnduzi ambap Zanzibar nzima ilikuwa na watu wapatao Laki 320 ambapo kwa hivi sasa idadi hiyo imeongezeka mara nne nako kumechangia kuongezeka kwa mahitaji yakiwemo yale ya usafiri.
Alisema kuwa kutokana na hatua hiyo ndio maana serikali haijalivunja Shirika lake la Meli la Zanzibar licha ya kutoa nafasi kwa wafanyabiashara kununua vyombo vya usafiri zikiwemo boti ziendazo kwa kasi pamoja na meli ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa wananchi.
Dk. Shein alisema kuwa madhumuni ya ziara hiyo ni kutoa mkono wa pole na kuwafariji wafiwa pamoja na kuwapa pole wale wote waliopata majeraha na kuahidi kuwa serikali itaendelea kuwasaidia na iko pamoja nao.
Aliendelea kutoa shukurani kwa wananchi wote wa Unguja na Pemba kwa utulivu, umoja, mshikamano na mapenzi makubwa waliyoonesha katika kipindi chote cha msiba huo sanjari na subira kubwa waliyonayo.
Dk. Shein alisema kuwa msiba huo ni wa watu wote, ni wa Wazanzibar an Watanzania wote kwa jumla kwani wote wamewaguswa na msiba huo.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa salamu za pole bado inaendelea kutolewa kutoka nchi mbali mbali duniani pamoja na Taasisi na Mashairika ya Kimataifa pamoja kuwaombea dua marehemu ambapo katika maelezo yake alioa salamu kutka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha -Rose Migiro ambazo zilieleza kuwa watanzania wanaoishi nchini Marekani walisoma hitma kwa kuwaombea dua ndugu zao waliopata msiba kutokana na tukio hilo.
Nao viongozi aliofatana nao Dk. Shein katika ziara yake hiyo walipata nafasi ya kutoa salamu zao za pole kw wafiwa na wale wote waliopoteza roho zao waliwaombea dua na wale waliopata majeraha waliwaombea dua kupona haraka.
Wafiwa nao walipata fursa ya kutoa shukurani zao kwar Rais Dk. Shein pamoja na Serikalimzote mbili kwa juhudi kubwa zilizochukuliwa tukio mwanzo wa msiba hadi hivi leo.
Wafiwa hao walieleza kufarajika kwao na jitihada za Dk. Shein za katika kukabiliana na tukio hilo na kutoa pongezi na shukurani kwa ziara yake hiyo ya kuwafariji wafiwa na kuwapa pole waliopata majeraha na kueleza kuwa hiyo yote ni mitihani ya MwenyeziMungu kwani viumbe wote hatimae watarejea kwake.
Tayari Dk. Shein ameshafanya ziara ya kuwafariji wafiwa na wale waliopata majeraha katika kisiwa cha Pemba, mpango ambao alisematayari ulikwisha andaliwa na serikali wa viomngozi wote wakuu akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye yeye alitangulia na Makamu wa Pili wa Rais ambaye hivi leo nae ameelekea kisiwani humo.