Dk Shein aanza ziara kuwashukuru Wazanzibari kumchagua

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ameanza kufanya ziara

katika baadhi ya maeneo ya Zanzibar akiwashukuru wananchi kwa kumchagua katika nafasi hiyo

kwenye uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.

Shein ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar tayari juzi amefanya

mikutano katika mikoa miwili ya Pemba huku akipangiwa kuendelea katika maeneo mengine.

Zifuatazo ni picha katika baadhi ya mikutano yake ya kuwashukuru wananchi.

Dk. Shein akizungumza na wananchi katika moja ya mikutano yake Pemba kuwashukuru wananchi kumchagua.