Dk. Nchimbi akizindua mnara wa kumbukumbu ya Mkutano wa TANU

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili mjini Bagamoyo alipoenda kuzindua Mnara wa kumbukumbu ya Mkutano wa Kwanza wa TANU kitaifa uliofanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius K. Nyerere Bagamoyo mwaka 1954 wakati wa harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika.( Kulia) ni Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Martin Shigella.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akipanda mti katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wana CCM wa mjini Bagamoyo baada ya kuzindua Mnara wa kumbukumbu kumbukumbu ya Mkutano wa Kwanza wa TANU kitaifa uliofanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius K. Nyerere Bagamoyo mwaka 1954 wakati wa harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika.

Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bagamoyo wakicheza kumkaribisha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi alipokwenda kuzindua Mnara wa kumbukumbu ya Mkutano wa Kwanza wa TANU kitaifa uliofanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius K. Nyerere mjini Bagamoyo katika harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika. (Picha zote na Lydia Churi wa Idara ya Habari-MAELEZO)