Dk. Mengi Ataka Wasambazaji Kushawishi Uwekezaji

Meneja Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda (kushoto) akitoa maelezo kuhusu ubora wa matrekta hayo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kushoto) alipotembelea kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 

MAKAMPUNI ya Tanzania ya uwakala wa usambazaji wa bidhaa za kutoka nje ya nchi, wameshauriwa kuyashawishi makampuni ya nje kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa hapa hapa nchini. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi ametoa ushauri huo jijini Dar es salaam wakati akitembelea mabanda ya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kutaka kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akielekea kukagua baadhi ya matrekta katika banda la Kampuni ya Agricom akiambatana na Meneja Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda (kulia kwa Dr.Mengi) alipotembelea kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Akifuatana na Mkurugenzi wa TPSF Bw. Louis Accaro, Afisa Biashara wa Tan-Trade Bw. Mohamed Mkadara, na Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wajasiriamali Bi. Jacquiline Maleko, Dr Mengi ametembelea mabanda mbalimbali, yakiwemo yaliyopo chini ya mwamvuli wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda, na Kilimo – TCCIA, Mfuko wa Fursa sawa kwa wote-EOTF, na Banda la Kampuni ya Agricom, ambayo Mkurugenzi wake Mtendaji Bi. Angelina Ngalula alielezea jinsi ilivyojipanga kusambaza zana za kisasa za kilimo ili kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji.

Katika majumuisho yake Dr Mengi alishauri Tan-Trade na TPSF washirikiane katika kuangalia namna ya kuboresha zaidi maonyesho hayo, hususan katika kuboresha mabanda ya maonyesho ili yalingane na hadhi halisi ya kimataifa.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agricom, Bi. Angelina Ngalula (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi alipotembelea banda la kampuni hiyo kujionea huduma zao kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 

Mratibu wa miradi na mshauri wa Maisha Finance Ltd, ambao ni wakopeshaji wa zana zote za kilimo yakiwemo Matrekta ya kampuni ya Agricom, Erasmus Erneus akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wateja, Apollos Rweikiza aliyetembelea banda la Agricom katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko (wa pili kushoto) alipowasili kwenye banda la TWCC yanakoendelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 

Mkurugenzi wa Fedha, Masoko na Usafirishaji wa C.E Holdings Ltd, wauzaji wa vito vya Afrika, Maria Pagama akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi alipotembelea banda la TWCC kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 

Picha juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akifurahia jambo na wanawake wafanyabiashara kwenye banda la TWCC katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha ya juu kulia ni Noreed Mawalla wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC).

 

Mkurugenzi wa Tanfood and Spice Co. Investment watengenezaji wa bidhaa za kutunza ngozi zinazotokana na mimea, Bi. Rona akitoa maelezo ya bidhaa halisi za kutunza ngozi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi alipotembelea banda la TWCC kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitoa maelekezo kwa Noreed Mawalla wa TWCC (katikati) wakati akitembelea banda la Chama cha wafanyabiashara wanawake kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitazama bidhaa mbalimbali katika banda la Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) lililopo katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

 

Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akimuongoza Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi mara baada ya kuwasili katika banda la EOTF kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Joane Art Craft, Culture & Desigin, Bi. Joane Baigana (kulia) alipotembelea banda la EOTF kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitazama kazi mbalimbali za wakinamama wajasiriamali kwenye banda la EOTF katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akisalimiana na wanawake wajasiriamali wanaofadhiliwa na EOTF akiendelea kutembelea wajasiriamali katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Anayemuongoza ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akisaini kitabu cha wageni katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu lililopo ndani ya banda la EOTF yanakoendelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitazama moja ya vitabu katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu lililopo ndani ya banda la EOTF. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akipata maelezo ya huduma mbalimbali za mikopo riba nafuu kwa wanawake kutoka kwa Afisa Huduma kwa Wateja wa Tanzania Women’s Bank, Renita Michael (kulia) ndani banda la EOTF wakati alipotembelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa na Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko.