Dk. Magufuli ‘Aunguruma’ Uwanja wa Tangamano Tanga…!

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Dk. Magufuli akisisitiza jambo mbele ya maelfu ya wananchi (hawapo pichani) kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika uwanja wa Tangamano.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Dk. Magufuli akisisitiza jambo mbele ya maelfu ya wananchi (hawapo pichani) kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika uwanja wa Tangamano.

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli akifafanua jambo mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Tanga waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni, uliofanyika katika viwanja vya Tangamano jioni ya Mjini Tanga.

  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tanga kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya angamano, jioni ya ambapo aliahidi kuboresha Bandari ya Tanga, kujenga Viwanda vya matunda na samaki ili kuweza kupunguza tatizo kubwa la ajira kwa vijana.

 Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, ambaye pia ni mgombea Ubunge viti maalum upande wa akina Mama mkoa wa Tanga (UWT),Ummy Mwalimu akimuombea Kura za kutosha mgombea Urais wa CCM Dk. Magufuli ili aweze kuibuka mshindi na kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.
 Wakazi wa Mji wa Tanga waliofika kwenye mkutano huo wakishangilia jambo.

 Nyomi la watu .

 Mgombea Urais wa CCM Dk. Magufuli akisalimiana na  Naibu Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba  Magharibi Mwigulu Nchemba
  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba akihutubia wakazi wa mji wa Tanga kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa Mji wa Tanga na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya Tangamano kwenye mkutano wa kampeni za CCM, ambapo Mgombea Urais wa CCM Dk. Magufuli aliwahutubia wananchi hao.
  Naibu Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba  Magharibi Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa Tanga mjini kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano.
  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba na Naibu Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba  Magharibi, Mwigulu Nchemba wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tangamano, ambapo Mgombea Urais wa CCM Dk. Magufuli alihutubia na Kumwaga sera zake kwa wananchi, ikiweno na kuomba ridhaa ya kuwaongoza katika miaka mitano ijayo.
 Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Mzee Yusuph Makamba akihutubia wakazi wa Tanga mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya viwanja vya Tangamano.
 Maelfu ya Wananchi wakimsikiliza Dk. Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kuwaomba wananchi hao wajitokeze kwa wingi Oktoba 25 na kumpigia kura ya ndio ili aibuke mshindi na kupewa ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.
 Mgombea Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa mji wa Tanga waliofika kwenye mkutano hadhara wa kampeni, uliofanyika jioni ya katika viwanja vya Tangamano mjini humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu. PICHA NA MICHUZI JR-TANGA