Dk. Magufuli Apokelewa kwa Shangwe Jimboni Kwake Chato

 Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki, mara baada ya kuwasili mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dk. Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dk. Magufuli.

  Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga Wananchi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuwashukuru kwa kiasi kikubwa kwa kuchaguliwa kwake katika nafasi ya kupeperusha bendera ya chama chake kuwania nafasi ya Urais .
 
  Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake waliokuwa wamekusanyika kwenye kituo cha mabasi wilayani humo wakishangilia kwa  furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dk. John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao.
 Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumlaki Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili mjini humo na shamra shamra za mapokezi kurindima kila kona wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dk. Magufuli, huku wengine wakiwa wamebeba mabango kama hivyo pichani.
   Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki, mara baada ya kuwasili mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dk. Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dk. Magufuli.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Ndugu Rajab Luhwavi akiwasalimia wanachama wa CCM pamoja na Wananchi waliofika kumlaki Dk. Magufuli katika kituo cha mabasi cha zamani ndani ya wilaya hiyo.
 Ilikuwa ni shangwe ndani ya Wilaya ya Chato ambako ndiko nyumbani kwa Mbunge na  Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dk. John Pombe Magufuli. 
   Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji  wa Katoro mkoani Geita alipokuwa akipita njiani kuelekea wilayani Chato. Kufuatia ujio wa Dk. Magufuli mkoani humo wananchi walijitokeza kwa wingi kila baada ya kilometa kadhaa na kuziba barabara wakita kumuona Dk. Magufuli na kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake na chama cha CCM.
 Mwananchi akiwa amekumbwa na joto la furaha mara baada ya kumuona Dk. Jonh Magufuli akiwa na msafara mzima wakielekea jimboni kwake Chato mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesse Mulongo akiwasalimia wananchi wa Chato kabla ya kumkaribisha Dk. John Magufuli aliyewasili mjini humo jana jioni ya akitokea mkoani Mwanza akijitambulisha kwa wananchi na kuwashukuru.
 Dk. Magufuli akizungumza jambo kwa maelfu ya wakazi wa mji wa Chato.
 Dk. Magufuli akifurahia jambo mbele ya umati wa watu, mara baada ya kujitambulisha kwao.
   Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wakazi wa mji huo kwa kujitokeza kwa wingi kumlaki, mara baada ya kuwasili mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dk. Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dk. Magufuli.
 Maelfu ya Watu walijitokeza kumlaki Dk. Magufuli mjini Chato mkoani Geita.
PICHA NA MICHUZI JR-CHATO-GEITA