Dk. Magufuli Akagua Barabara ya Kilwa Dar

Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli akijiridhisha kwa kupima kiwango cha lami inayowekwa upya katika barabara ya Kilwa na Kampuni ya Kajima ya Japan jijini Dar es Salaam. Wengine wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki, Balozi wa Japani nchini Tanzania Masaki Okada na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Kajima. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli (mbele) akiwa amefuatana na balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na viongozi wengine wa wizara akikagua moja ya sehemu ya barabara ya Kilwa inayojengwa upya na kampuni ya KAJIMA ya Japan kutokana na barabara hiyo iliyokamilika hapo awali kuwa chini ya kiwango na Serikali ya Tanzania kuikataa na kuiagiza kampuni hiyo iijenge upya kwa gharama zake. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

Wafanyakazi wakiendelea na ujenzi wa barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli akikagua ujenzi wa daraja la Kigamboni akiwa ameambatana na viongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Mecki Sadiki (wa pili kutoka kulia) Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndugalile (wa tatu kutoka kulia) jijini Dar es Salaam. Daraja la Kigamboni linajengwa na kampuni ya China Railways Engineering kwa gharama ya sh. bilioni 214 na linatarajia kukamilika kabla ya mwaka 2015. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.