Dk Magufuli Atema Cheche, Kuanza na Watendaji Serikalini

Rais mteule wa Tanzania anayesubiri kuapishwa, Dk. John Magufuli akizungumza leo.

Rais mteule wa Tanzania anayesubiri kuapishwa, Dk. John Magufuli akizungumza leo.

Rais mteule wa Tanzania anayesubiri kuapishwa, Dk. John Magufuli akizungumza leo.

Rais mteule wa Tanzania anayesubiri kuapishwa, Dk. John Magufuli akizungumza leo.

RAIS mteule wa Tanzania anayesubiri kuapishwa, Dk. John Magufuli amewataka wantendaji wa Serikali wasiopenda kujituma, wazembe na wavivu waanze kujipanga kwani katika utawala wake hawezi kuwavumilia atafukuza mmoja baada ya mwingine na kubaki na wanaotaka kufanya kazi kwa kujituma.

Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam akizungumza kutoa shukrani kwa baadhi ya wananchi na WanaCCM waliofika kwenye mapokezi ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizopo Mtaa wa Lumumba. Wananchi hao walifika kumpokea akitokea Ukumbi wa Diamond Jubilee alipokabidhiwa hati ya uteuzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) siku moja baada ya kutangazwa msindi wa nafasi hiyo.

Alisema anajisikia ni mwenye deni kwa Watanzania kwa uaminifu mkubwa waliuonesha kwake, hivyo kuona anachangamoto kubwa zaidi ya kufurahia ushindi alioupata. “…Mimi mwenzenu sijafurahi sana…Maana naiona changamoto, mjue kuna watu nitawagusa waliozoea kuishi kwa mazoea huenda wasifurahi. Lakini ili jipu lipone lazima lipasuliwe na damu itoke,” alisema Dk. Magufuli.

Dk. Magufuli amewataka wanachama wa CCM kushirikiana katika kukijenga na kukiendeleza chama kwani uchaguzi umekwisha. Aliwataka baadhi ya wanachama kuacha unafiki na kukwamishana katika mipango ya maendeleo kwani hata wavumilia kamailivyozoeleka.

“…Yaani ni heri ubaki na wanachama wachache watiifu kuliko wanafiki ndani ya chama. Mwenyekiti wangu naomba unisamehe, ulikua na wanafiki na wasaliti ndani ya chama chetu waliotukwamisha hadi tumefikia hapa..Ni heri uwe na mchawi kuliko wanafiki,” alisema Dk. Magufuli.

Baadhi ya wanaCCM wakimsikiliza Dk. John Magufuli akizungumza.

Baadhi ya wanaCCM wakimsikiliza Dk. John Magufuli akizungumza.

Aliwashukuru wanaCCM kwa umoja wao ambapo waliutafuta ushindi kwa nguvu zote, hivyo kuwaomba wampe ushirikiano wao katika kutekeleza yale aliyoahidi maana bila ushirikiano kasi ya utekelezaji itakuwa ndogo.

Yeye hatavumilia Wanafiki na amemuomba Mwenyekiti asafishe Chama kabla ya kumkabidhi. Amesema katika kutumbua jipu ni lazima damu itoke kidogo. Wanafiki wajue kuwa yeye hatakuwa na huruma nao ni bora kuwa na wana CCM wachache wazuri kuliko wanafiki wengi. Aliongeza kuwa wanaCCM lazima waelezane ukweli kwani ndani ya CCM kuna wanafiki ambao wamekuwa wakikihujumu chama.

Aidha amewashukuru Watanzania wote waliomchagua kwa kiasi kikubwa kwani hata maeneo mengine ambapo mbunge au diwani wa CCM hakichaguliwa laki yeye alichaguliwa kwa kura nyingi kuonesha kuwa wanaimani kwake na kwa CCM.