Dk Laurent Shirima Ateuliwa Mtendaji Mkuu wa PPRA

Dk Laurent Shirima Ateuliwa Mtendaji Mkuu wa PPRA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dk Laurent M. Shirima kuwa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA).

Dk. Shirima alikuwa ni Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo wa Huduma za Ushauri (Capacity Building and Advisory Service-PPRA) na pia ndiye aliyekuwa akikaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa PPRA.

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2014.