Dk. Bilal mgeni rasmi Maadhimisho Miaka 35 ya Reli ya Tazara

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yamefanyika leo Septemba 14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Tazara, Mkandarasi Abdallah Shekimweri, kuhusu matumizi ya Kibelenge wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya TAZARA kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yalifanyika leo Septemba 14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka katika moja ya mfano wa Behewa la Daraja la kwanza la Treni ya TAZARA, wakati alipokuwa katika maonyesho ya TAZARA, wakati wa maadhimisho ya miaka 35 ya shirika hilo sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, iliyofanyika katika viwanja vya TAZARA jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR