Dk. Bilal kwenye mkesha wa sherehe za Maulid

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, wakati wakiwa katika sherehe za mkesha wa Maulid, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, jana usiku Februari 04, 2012, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika shambrashambra za mkesha wa sherehe za Maulid, jijini Dar es Salaam jana Februari 04, 2012 usiku. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Muumin wa dini ya kiislam kutoka Msikiti wa Suni Hanafi wa jijini Dar es Salaam, Muzamil Chaki, baada ya muumini huyo kumaliza kutoa burudani ya Qaswaida jukwaani, wakati wa mkesha wa sherehe za Mauilid zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini jana usiku Februari 04, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR