Dk. Bilal, JK wahudhuria hafla ya kusainiwa mkataba wa kupambana na maharamia kiushirikiano kati ya Tanzania, Msumbiji na Afrika Kusini

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dk. Mohammed Gharib Bilal (nyuma) wakishuhudia zoezi la utiaji saini wakati Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Husein Mwinyi, akisaini mkataba wa makubaliano (MoU) ya Ushirikiano katika mapambano dhidi ya Maharamia

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Ghalib Bilali washuhudia Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyarusi (shoto)na wa Tanzania Dk. Hussein Mwinyi wakibadilishana nyaraka huku wa Afrika Kusini Dk. L.N. Sisulu akitazama baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao. Picha na Ikulu.

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Ghalib Bilal wakiwa katika picha ya pamoja na na Mawaziri wa ulinzi wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyarusi (shoto), wa Afrika Kusini Dk. L.N. Sisulu na wa Tanzania Dk. Hussein Mwinyi baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.