Dk Bilal azungumza na Watanzania waishio Burundi


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwaaga baadhi ya Watanzania waishio Burundi baada ya kumaliza mazungumzo alipokutana nao Bujumbura Burundi Novemba 30 na kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Watanzania waishio Bujumbura Burundi, baada ya kumaliza mazungumzo baina yao yaliyofanyika jana Novemba 30 na kujadili mambo mbalimbali yanaoendelea katika Taifa la Tanzania.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati alipokutana na Watanzania waishio nchini Burundi jana Novemba 30. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Mwasi Nzagi (kulia) ni Mwenyekiti wa Kinamama wa Jumuiya ya Kinamama waishio Burundi, Siwajibu Hamis (wa pili kulia) ni Mwenyekiti wa Vijana wa Jumuiya hiyo, Mutalemwa Julian. (Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR)