Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma, wakati alipotembelea katika chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring System) baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa. Picha na OMR