Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Daraja la Mingumbi lililopo Wilaya ya Kilwa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi Januari 22, 2012. Kushoto ni mkewe, Mama Zakhia Bilal (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea maeneo ya Shule ya Sekondari ya Ilulu, wakati alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuzindua Jengo jipya la Bwalo la Shule ya Sekondari ya wasichana, Ilulu, iliyopo Kilwa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoa wa Lindi Januari 22, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikagua ujenzi wa jengo la Zahanati ya Kilanjelanje iliyopo Jimbo la Kilwa Kusini, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi Januari 22, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Na Mwandishi Wetu, Lindi
MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal anayeendelea na ziara yake mikoa ya Kusini ameweka mawe ya msingi ikiwa ni pamoja na kuzindua miradi mitano katika maeneo tofauti ya mikoa hiyo.
Jana Dk. Bilal amezindua miradi mitano ambayo ni pamoja na kuweka jiwe la Msingi katika jengo la Kituo cha Afya cha Kitomanga lililopo Lindi Vijijini, uzinduzi wa Daraja la Mingumbi Kilwa, pamoja na uzinduzi wa jengo jipya la Bwalo la Shule ya Sekondari ya wasichana, Ilulu, iliyopo Kilwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jilwe la msingi katika Ofisi mpya ya Chama cha Mapinduzi CCM, iliyopo Chumo Namkamba Kilwa Januari 22, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoa wa Lindi. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Miradi mingine ni pamoja na kuweka jilwe la msingi katika Ofisi mpya ya Chama cha Mapinduzi CCM, iliyopo Chumo Namkamba Kilwa, kukagua ujenzi wa jengo la Zahanati ya Kilanjelanje iliyopo Jimbo la Kilwa Kusini na shughuli nyingine za maendeleo.
Zifuatazo ni picha za matukio ya shughuli mbalimbali alizozifanya Dk. Bilal na viongozi wenyeji wa Mkoa wa Lindi, ambao umekuwa na changamoto kadhaa kimaendeleo ya kiuchumi kwa muda sasa.