Dk. Bilal azindua Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kumbukumbu ya Kigoda cha Mwalimu Nyerere kinachohusika na masuala ya Mazingira na mabadiliko ya Tabianchi, kilichozinduliwa Julai 11, 2011 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutangazwa kwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda hicho, Prof. Pius Yanda. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rwekaza Mukanda (kulia) akimvisha kofia na Joho, Prof. Pius Yanda, baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu yerere, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kigoda hicho kilichozinduliwa kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Julai 11, 2011. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Makenya Maboko.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Prof. Pius Yanda, baada ya kutangazwa na kuvishwa Joho la kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kigoda hicho uliofanyika leo Julai 11, 2011 katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Mkurugenzi na Kiongozi wa Bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto, akiigiza kusafiri na Ngamia wake, wakati akitoa burudani ya kuimba mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere kilichozinduliwa leo Julai 11, 2011 Chuo Kikuu Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikagua maonesho ya vitabu vya kumbukumbu nje ya ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kuzinduz Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki na maprofesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya uzinduzi huo. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR