Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Jengo la Mihadhara na kuchangisha fedha za ujenzi wa Maabara ya Shule ya Sekondari Chang’ombe, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE jijini Dar es Salaam Septemba 13, 2011. Kusho ni mwakilishi wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDSM, Prof. Yunus Mgaya na (kulia) ni Mkuu wa Chuo hicho Kikuu Kishiriki cha DUCE, Prof. Salome Misana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal (katikati) akipata maelezo ya awali kutoka kwa mkuu wa Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Prof. Salome Misana kuhusu jengo jipya la mihadhara lililopo chuoni hapo ambalo lina uwezo wa kuchukua wanachuo 2,000 kwa wakati mmoja. (Picha na Aron Msigwa –MAELEZO)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, Prof. Salome Misana, baada ya kuzindua rasmi Jengo la Mihadhara la chuo hicho na kuendesha zoezi la uchangishaji fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Maabala ya Shule ya Sekondari Chang’ombe jijini Dar es Salaam Septemba 13. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Jengo jipya la mihadhara la Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kama linavyoonekana kwa nje ambalo limezinduliwa jana na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal (Picha na Aron Msigwa –MAELEZO)