Dk. Bilal awazawadia washindi wa kuhifadhi Qur-an


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa fainali wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, Jahuddi n Adam, kutoka Sudan, baada ya kutangazwa mshindi wa fainali hizo, zilizofanyika Agosti 21 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, wakati wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, zilizofanyika leo Agosti 21 kwenye ukumbi wa Diamondi Jubilee jijini Dar es Salaam, na kuwashirikisha washiriki 14, kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.


Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye alishika nafasi ya pili katika mashindano hayo, Kombo Bahi Makame kutoka Unguja-Tanzania, akishiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo Agosti 21, ambapo mgeni rasmi katika fainali hiyo iliyowashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na kati, alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu, wakiwa katika picha ya pamoja na washindi wa kwanza hadi wa tatu wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, baada ya kutangazwa washindi hao katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 21.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, baada ya kumalizika kwa mashindano hayo katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 21.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma Hotuba yake wakati wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo Agosti 21, na kushirikisha jumla ya wshiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati. (Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR)