Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Mtemi na Chief Mkuu wa Kijiji cha Inyonga, George Mbaula (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Machief wa Inyonga, baada ya kumvisha nguo za asili ya Kabila la Kikonongo na kumkabidhi mikoba ya kuwa Chifu wa Kabila hilo, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa Februari 19, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu Wa Rais wa Jamhuti ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa na mavazi ya asili ya kabila la Kikonongo baada ya kuvishwa na kutunukiwa uchifu wa Kabila la Kikonongo na machifu wa Kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mpanda wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi Februari 19, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu a Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Inyonga Mkoa wa Katavi wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa katavi Februari 19, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea shamba ufugaji wa Nyuki wa kisasa la Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lililopo Kijiji cha Vilolo wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa Februari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Baba mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Exavery Kayanza Pinda, wakati alipokuwa akipita kuelekea Kijiji cha Mwamapuli akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi, Februari 20. 2012. Kulia nia Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Eng. Stella Manyanya. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal, akisalimiana na Mama mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Albetina Kasanga, wakati wakiwa katika ziara ya Mkoa wa Katavi Februari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR