Dk. Bilal apokea mchango wa Wachina kwa waathirika wa mafuriko

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 10, kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina wa Tanzania (CBCT) kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam Januari 15. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal jana alipokea mchango wa sh. milioni 10 ukiwa ni mchango toka kwa Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina wa Tanzania (CBCT) kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba 2011.

Mfano huo wa hundi ya sh. milioni 10 ulitolewa jana na akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 10, kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 16, kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na City Bank Tanzania LTD kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam Januari 15. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


Dk. Bilal ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT), pia alipokea hundi ya sh. milioni 16 kutoka City Bank Tanzania LTD kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam.

Sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT) zimefanyika jana jioni kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni anuai, zikipambwa na burudani kedekede kutoka kwa wasanii wa Kichina.