Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mkulima wa Nyanya, Judith Munis, wa Kikundi cha Upendo Jegestal, kuhusu kilimo cha nyanya, wakati alipotembelea wakulima wa Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha Jegestal-Lushoto, Januari 27, 2012, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasalimia na kuwaaga wasanii waliokuwa wakitoa burudani, wakati akiondoka Chakechake baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Januari 27, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Tanga. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wakulima wa mbogamboga, Juma Kambaga, kuhusu uzalishwaji wa mbogamboga hizo wakati alipotembelea wakulima wa Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha Jegestal-Lushoto, jana Januari 27, 2012, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia chupa ya Juisi iliyotengenezwa na wajasiliamali, Salome Mtawa (kulia) wa kikundi cha Usambara Lishe Trust, wakati alipotembelea wakulima wa Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha Jegestal-Lushoto, Januari 27, 2012, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga. Picha na Muhidin Sufiani-OMR