Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya wananchi waliohifadhiwa katika Kambi ya Shule ya Sekondari ya Azania, waliookolewa katika maeneo yaliyojaa maji kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa pole wananchi hao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo ya jinsi maji yalivyokuwa yamejaa wakati wa mvua kubwa iliyosababisha mafuriko, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick (kulia), wakati alipotembelea kuwapa pole wananchi waliokuwa wamehifhadhiwa katika Klabu ya Yanga, iliyopo Jangwani Desemba 23. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR