Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Mabalozi wateule wanaokwenda kufanya kazi nchi za nje walizopangiwa, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga kabla ya kwenda kuanza majukumu yao ya kikazi katika nchi walizopangiwa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, aliyefika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini. Picha na Muhidin Sufiani-OMR