Dk. Bilal akabidhi zawadi kwa washindi mashindano ya Qur-an


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 30, Mariam Salum Mohamed (15) kutoka Tarbiyatul-Islamiyah Pemba, aliyeibuka na jumla ya Pointi 97 katika mashindano hayo yaliyofanyika Agosti 14 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kuliani ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake, Baraza Kuu la Kiislam (BAKWATA), Shamim Khan, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam Agost 14. Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 30, Shaame Said Shaame (18) kutoka, Ibun Jazary Vikindu, aliyeibuka na jumla ya Pointi 93 katika mashindano hayo yaliyofanyika Agosti 14 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa fainali za mashindano ya Qur-an kuhifadhi Juzuu 30, zilizofanyika Agosti 14 kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Mshindi wa kwanza katika fainali hizo alikuwa ni Mariam Salum Mohamed, kutoka Tarbiyatul-Islamiyah Pemba. Picha na Muhidin Sufiani-OMR