Dk Bilal Aitaka TBA Kuangalia Fursa na Kujenga Nyumba za Watumishi wa Umma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga, wakati akikagua ramani za ujenzi wa Makazi ya Nyumba 851  za Watumishi wa Umma zinazojengwa katika eneo la Bunju B, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, wakati wa sherehe hiyo liyofanyika leo. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba 851 za Watumishi wa Umma zinazojengwa katika eneo la Bunju B, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, wakati wa sherehe hiyo liyofanyika leo. Kutoka (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Miundombinu, Peter Serukamba, Waziri wa Ujnezi, Dkt. John Pombe Magufuli na (kushoto) kwa Makamu ni Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga na Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi. Picha na OMR

Na Eliphace Marwa – MAELEZO

MAKAMU wa Rais Dk. Mohamed Ghalib Bilal ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuangalia jinsi ya kutumia fursa amabayo Serikali imeruhusu taasisi za Serikali kuingia ubia ba sekta binafsi (PPP) katika kufanikisha miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais wakati sherehe za uweka ji wa jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 851 za watumishi wa umma katika eneo la Bunju B, wilaya ya kinondoni Jijini Dar es Salaam.

“Wakala mnatakiwa muangalie jinsi ya mtakavyoweza kutumia wabia wa ndani na wa nje katika kutekeleza mradi maalum wa ujenzi wa nyumba 10,000 kwa kipindi cha miaka mitano  ambao unatazamiwa kutatua kero ya makazi ya watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla,” alisema Dk. Bilal.

Makamu wa Rais aliongeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kazi bora inayofanywa na watumishi wake ndiyo maana inawaonesha kuwajali kwa kuwajengea nyumba bora.

Aidha aliupongeza wakala huo, kwa kuanzisha mradi huo wa kujenga nyumba hizo, ambapo  gharama ya nchini inaanzia milioni 25 hadi kufikia milioni 50.

Naye Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli akielezea changamoto mbalimbali ambazo wakala huo, unaakabiliana nazo kuwa ni gharama kubwa za uwekaji miundombinu ya maji safi na nishati.

Alizitaja changamoto nyingine ni kutozwa riba kubwa za mikopo zinazotolewa na benki za hapa nchini, pia baadhi ya halimashauri kutokuwa na viwanja vya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.

“Naomba Makamu wa Rais na ofisi yako inisaidie kuhakikisha wale wote ambao wanadaiwa mikopo ya nyumba wawe wamelipa ndani ya mwezi mmoja ikiwa watashindwa kulipa wanyang’anywe nyumba hizo na kuuziwa watu wengine ili kutoa fursa kwa wakala kujenga nyumba nyingine, ambapo hadi sasa watu 2500 bado hawajamaliza kulipa madeni yao,” alisema Waziri Magufuli.

Aidha wakala huo, utajenga nyumba nyingine 1400 katika mkoa wa Dares Salaam na nyumba 2500 katika mikoa 12 ya Tanzania Bara kwa kipindi cha mwaka huu wa fedha wa 2013/2014 na kumalizia nyumba zilizo baki ndani ya miaka mitatu, ambapo Makamu wa Rais alitaka ujenzi huo usisimame ili kufikia lengo la nyumba 10,000 na zaidi.