Dk. Bilal afungua onesho maalumu la Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam Novemba 8, kufungua onyesho la maalum la Vyombo vya Ulinzi na Usalama (VUU) lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Watanzania kwa kudumisha amani na Umoja katika kuelekea Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Onesho maalum la Vyombo vya Ulinzi na Usalama (VUU) lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Watanzania kwa kudumisha amani na Umoja katika kuelekea Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Onesho hilo lilifanyika Novemba 8 katika Ukumbi wa Diamond jubilee Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Polisi, wakionyesha umahiri wao jukwaani wakati wa Onesho maalum la Vyombo vya Ulinzi na Usalama (VUU) lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Watanzania kwa kudumisha amani na Umoja katika kuelekea Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam Novemba 8. ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal. Picha na Muhidin Sufiani-OMR