Dk. Alberic Kacou azindua Ripoti ya Dunia ya Uwekezaji 2012

Pichani Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Dunia ya Uwekezaji 2012 yenye kauli mbiu ‘Sera Kuelekea Kizazi Kipya katika Uwekezaji’ ambapo amewasisitiza watunga sera wa Tanzania kutumia rasimu ya Sera ya Uwekezaji ya Maendeleo Endelevu kwa mwaka 2012 kama kipaumbele katika kuunda sera za Kitaifa za Uwekezaji. Kushoto ni Ofisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC) Bi. Stella Vuzo.

 

Baadhi ya Maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini waliohudhuria uzinduzi wa World Investment Report 2012.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Raymond Mbilinyi akiwasilisha Ripoti hiyo ya Mwaka 2012 ambapo amezungumzia zaidi mazingira ya uwekezaji Tanzania huku akigusia mwelekeo, changamoto na fursa zinazopatikana.

Bw. Raymond Mbilinyi ameweka wazi kuwa mujibu wa Ripoti hiyo Tanzania kwa sasa imepiga hatua katika kuboresha miundo mbinu haswa ya Barabara miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.

Dkt. Alberic Kacou (kushoto) na wadau wakifuatilia uwasilishwaji wa Ripoti ya Fursa za Uwekezaji 2012.

Pichani ni Minongoni mwa Mabalozi, wawakilishi wa Serikali, wakuu wa mashirika ya Maendeleo, wawakilishi wa mashirika ya kijamii katika uzinduzi huo.

Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akimkaribisha Dkt. Kacou na Bw. Mbilinyi (hawapo pichani) kuzindua rasmi ‘World Investment Report 2012’.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Raymond Mbilinyi (kulia) akikata utepe kuzindua kitabu chenye Ripoti ya Uwekezaji ya Kimataifa 2012 sambamba na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou.

Sasa imezinduliwa rasmi.

Na Mwandishi wetu
BENKI ya Twiga Bancorp, imezindua huduma mpya ya kukusanya maoni ya wateja wa ndani na nje ya Tanzania ili kutathimini utoaji huduma wa benki hiyo. MKurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Mawasiliano ya Kompyuta wa Benki hiyo, Richard Kombole, aliyasema hayo Dar es Salaam jana, alipozungumzia kuzinduliwa kwa huduma hiyo itakayokuwa endelevu.

Alisema wakati huu ambapo benki hiyo imekuwa inajitanua kwa kufungua matawi mbalimbali nchini, kumeonekana ulazima kwa benki kupata maoni ya wananchi kuhusiana na huduma za benki hiyo ili kuongeza ufanisi.

“Hivi juzi tulipata tuzo ya dhahabu ya kimataifa ya utoaji wa huduma bora. Hii inatupa ishara kwamba katika ngazi ya kimataifa, huduma zetu zinakubalika na kuheshimika tumeona kula ulazima wa kukusanya maoni kwa wateja wetu wa ndani,” alisema Kombole.

Alisema ikiwa na ushirikiano na benki zaidi ya 24 zenye mashine za ATM 160 nchi nzima kupitia huduma ya Umoja Switch, Twiga Bancorp imeendelea kujitanua kwa kufungua matawi katika Mikoa ya Arusha na Mwanza na karibuni itafungua tawi jipya mkoani Dodoma.

Alisema katika kuwezesha hilo, benki hiyo itatawanya fomu maalumu za kukusanya maoni ya wateja juu ya utolewaji wa huduma ambayo yatafanyiwa kazi mara moja baada ya kupokelewa.

“Katika hili mteja wetu atakuwa huru kutoa maoni yake katika suala lolote lile linaloihusu benki yetu bila ya kuwa na hofu kwani bila kuwepo kwa wateja benki yetu haiwezi kuwepo,” alisema Mkurugenzi huyo.

Katika hatua nyingine, Benki hiyo ipo katika mchakato wa kuboresha huduma za kibenki kwa kufunga mitambo ya kisasa ya kompyuta ili kuiwezesha kutoa huduma kwa mawasiliano ya kompyuta za benki hiyo na benki nyingine bila kumlazimu mteja kwenda benki.

Akizungumzia mpango huo, Kombole alisema unatarajia kukamilika na kuanza kazi Aprili mwakani ambapo wateja watatakiwa kuwasilisha taarifa zao binafsi ili kuwawezesha kuingizwa katika mfumo huo mpya wa digitali.

“Hii itatuwezesha kuweza pia kuwasiliana kirahisi na wateja wetu litakapojitokeza jambo lolote kama vile kubadilika kwa namba za akaunti au matatizo katika akaunti ya mteja bila mteja kulazimika kuja benki,” alisema Kombole.