Dili la Simba Kumnasa Hemed Morocco Limebuma

Nembo ya Simba

Klabu ya SimbaSC ilikuwa kwenye mazungumzo ya kumpa kazi ya u-technical director kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Hemed Suleiman Ally ‘Morocco’, dili hilo lemeenda mrama baada ya wekundu wa Msimbazi kushindwa kuafikiana na Morocco juu ya kiwango cha mshahara.

Mwanzoni Morocco alikubaliana na uongozi wa Simba tangu wakiwa visiwani Zanzibar wakati Simba ilipokuwa ikishiriki mashindano ya Mapinduzi hadi Morocco akafunga safari ya kuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuja kumalizia vipengele vichache ili ajiunge na timu.Lakini ghafla uongozi wa Simba ukabadili maamuzi ya kiwango cha mshahara ambao walikuwa wamekubaliana mwazo.

IMG-20160119-WA0015

Morocco alikubaliana na uongozi wa Simba kwamba, watakuwa wakimlipa Tsh. 5,000,000 kwa mwezi, lakini baadaye wakabadilisha maamuzi na kumwambia Morocco watakuwa wakimlipa Tsh. 4,000,000 kwa mwezi. Kuona hivyo Morocco akaamua kupiga chini dili hilo kutokana na uongozi wa Simba kupunguza kiwango cha mshahara wake kwa mwezi.

Kutokana na Morocco kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa, TFF tayari walishampa ruhusa ya kwenda kufanya kazi Simba kwa barua rasmi.