Diaspora World Cup: Tanzania yatoka sare na Ethiopia

Kikosi kamili cha timu ya waTanzania DMV wakiwa na mdhamini mpya wa timu hiyo Mbunifu wa mitindo ya Kwetu Missy Temeke, pamoja na shabiki Didi Vava, katika uwanja wa Greencastle, uliopo Burtonsville, Maryland

Mchezaji wa timu ya Ethiopia akipambana vikali na Yousouf Godson Liuzinho wa Tanzania, kipindi cha kwanza kwenye mchezo huo wa Ligi ya 2011 Diaspora World Cup uliofanyika kwenye kiwanja cha Greencastle, cha Burtonsville, Maryland.

Mdhamini mpya wa timu ya wa Tanzania DMV ambaye ni mwanamitindo na mbunifu wa mitindo ya (Kwetu Fashion Design), Missy Tetemeke akijivinjali na flagi la nchi na timu yake uwanjani alipokuwa akifuatilia mpambano huo.

Wachezaji wa Ethiopia wakijipanga kupiga mpira wa adhabu katika dakika ya 62 ya mchezo huo.

Didi Vava (kushoto) akiwa na Sharif Qullatein, Dogo Hudhaifa Shatry, na Mmiliki wa Blog ya Swahilivilla Abou Shatry katika jukwa la wapenzi wa timu ya Watanzania DMV. Timu hizo zilitoka sare ya bila magoli mashindano ya Ligi ya 2011 Diaspora World Cup.

Benchi la akiba la Timu ya Watanzania DMV wakiwa wanaangalia mchezo huo ulivyokwenda dhiti ya Timu ya Waethiopia

Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Ethiopia ya Maryland U.S wakiwa bechi. Picha zote na Abou Shatry wa swahilivilla.blogspot.com