Dewji Atoa Milion 78 kwa Viongozi wa CCM Ili Kutekeleza Ilani

Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mh. Mohammed Gullam Dewji akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kituo cha mabasi cha zamani mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).

E83A0131

 

E83A0112

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kuzungumza na wananchi wa jimbo lake.

E83A0094

Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mh. Mohammed Gullam Dewji, akiwa anasalimiana na Wana CCM na wananchi wa Singida mjini kwenye kituo cha mabasi cha zamani mjini Singida.

Na Nathaniel Limu.

Mbunge wa Singida mjini (CCM) Mh. Mohammed Gullam Dewji amemwaga misaada mbalimbali ikiwemo kuwaongezea mitaji wauza kahawa chungu, ambayo haijawahi kutolewa jimboni humo na mbunge au mfadhili yeyote kwa wakati mmoja, kabla na baada ya Tanzania kupata uhuru.

Misaada hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87.9, ni pamoja na mabati 100 na mifuko ya saruji 100, kwa kila shule 17 za sekondari jimboni humo.

Misaada mingine ni vyereheni viwili kwa kila kata 19  na cherehani moja kwa kila tawi la CCM jimboni humo.

Pia vikundi 16 vya wajasiriamali vikiwemo vya kung’arisha viatu, mafundi baiskeli, wapiga debe wa vituo vya mabasi, wasukuma matoroli, wakereketwa wa mashina ya CCM, watengeneza viatu vya kienyeji na baba, mama lishe, kila kimoja kimeongezewa mtaji wa shilingi 500,000 taslimu.

Vifaa hivyo na mitaji ya biashara, vimetolewa kwenye mkutano  wa hadhara uliofanyika kwenye kituo cha zamani cha mabasi mjini Singida.

Akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wana-CCM na wananchi kwa ujumla, Mh. Dewji amesema msaada huo ni mwendelezo wa misaada yake anayoitoa kwa ajili ya kuiunga mkono serikali katika kuwatumikia wananchi.

Amesema pia kuwa misaada hiyo ni sehemu yake ya utekelezaji wa ilani ya CCM  katika kuwatumikia wananchi wa jimbo la Singida mjini.

Amesema “Tunatakiwa tujitume usiku na mchana, ili tuhakikishe  kila tuliyoyaahidi kwenye ilani yetu, yote tumeyakamilisha, vinginevyo wananchi hawatatuelewa. Wananchi wanahitaji utimilifu wa ahadi na sio uhodari wa  kujieleza kwenye majukwaa”.

Katika hatua nyingine, Mh. Dewji ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi na watendaji kuendelea na moyo safi wa kuwatumikia wananchi bila kuchoka.

Amesema pia wawe waaminifu na waadilifu kwa wananchi na waongozwe kwa dhamira iliyo njema, yenye uzalendo wa kuipenda nchi yetu na watu wake.

Mbunge Dewji amesema “Tuendelee kuhubiri amani na utulivu kwenye majukwaa, wakati wote tuwaelekeze wananchi kwenye kujiletea maendeleo endelevu ya wakati huu na wakati ujao”.