Yohane Gervas, Rombo
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Siprian Kiwango, mwenye umri kati ya miaka 60-70 mkazi wa
Shimbi amefariki dunia papo hapo baada ya pikipiki aliyokua akiendesha kugongana na gari ndogo.
Taarifa ya Polisi iliyotolewa kwa waandishi wa habari mjini hapa inaeleza kuwa, ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nane mchana ikihusisha gari aina ya suzuki lenye namba za usajili T 771 CKE na pikipiki yenye namba za usajili T 659 AVX.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni mwendokasi wa gari hilo. Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa hata hivyo dereva wa gari alionekana mlevi na hivyo kushindwa kumudu gari lake hali iliyomfanya kukosa uelekeo kabla ya kusababisha ajali hiyo.
Akizungumza mmoja wa shuhuda wa ajali hiyo aliwataka madereva kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali ambazo zinaweza kuzuilika.