MWENDESHA bodaboda John Choma miaka (29) mkazi wa Majengo mapya Halmashauri ya Mji wa Mpanda mkoani Katavi amenusulika kifo baada ya kuchomwa kisu tumboni na mtu aliyetaka kumpora pikipiki, hali yake ni mbaya hivyo amepelekwa kwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoania Katavi Dhahiri Kidavashari ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Disemba 21 majira ya saa kumi usiku maeneo ya makaburi ya waarabu eneo la madukani. Kamanda Kidavashari amasema kuwa Dereva huyo wa bodaboda alikuwa akiendesha Pikipiki yenye namba za usajili T685 CWN aina ya SLG alikuwa amembeba abilia aliyepakia eneo la Makanyagio kwenye nyumba ya kulala wageni ya South Loji.
Alipofika eneo la makaburi alimwambia amushushe alipomshusha alimmchoma kisu kwa lengo la kutaka kumpora pikipiki lakini hakufanikiwa kwa kuwa mwendesha huyo pikipiki alipiga kelele na watu wakajitokeza kumsaidia kwa kukwa ilikuwa karibu na nyumba kisha Mharifu huyo alikimbia ingawa kijana yule alieleza kuwa aliweza kumtambua kwa mchomaji huyo kwa sura.
Kumekuwepo na matukio ya mauaji na uchomaji wa vifo kwa madereva pikipiki ambapo Wiki mbili zilizopita Mwendesha Bodaboda mwingine Zakari Lungwamiaka (24) aliuwawa kwa kuchomwa kisu tumboni na abiria aliyekuwa amembeba kwa lengo la kutaka kupora Pikipiki.