uzinduzi wa mradi huo.
KITUO cha Utamaduni na Maendeleo cha Denmark (CKU), kimetoa msaada wa vifaa vya muziki katika Tasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo (TASUBA) vyenye thamani ya shilingi milioni 80 za kitanzania.
Mbali na kununua vifaa vya muziki, sehemu ya fedha hizo pia zitatumika katika matengenezo na usimamizi wa
vifaa hivyo kwa kipindi cha mwaka mmoja wa mradi huo.
Akizungumza jana wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Msimamizi wa program CKU hapa Nchini, Mandolin Kahindi anasema kuwa ni moja fursa ya kuendeleza utamaduni na maendeleo ya kiuchumi.
Alisema kuwa msaada huo ni utekelezaji wa mpango wa utamaduni na ubunifu Tanzania inayotekelezwa na kituo hicho kwa ushirikiano na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
“Unajua mpango wa kuanza kutoa msaada Tasuba ulianza mwaka 2014 baada ya CKU kukitembelea chuo hicho na kuelezwa kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa vifaa vya muziki vya kufundishia na
kujifunzia,” alisema.
Alifafanua kuwa mpango huu wa kusaidia uliazinduliwa rasmi juni mwaka jana ililenga kutengeneza fursa za kiuchumi kupitia jukwaa la sanaa na ubunifu ambapo watanzania watajipambanua kupitia kushiriki shughuli mbalimbali za kitamaduni na kujipatia kipato.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Kutoka Wizara ya Habari, utamaduni, sanaa, na michezo Leah Kihimbi alisema kuwa amefurahi kupata msaada huo katika chuo cha sanaa lengo likiwa ni
kuendeleza vipaji hapa nchini.
“Katika chuo hiki ni kweli kulikuwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia lakini sasa tumepokea msaada kutoka
katika Danish Centre for Culture and Development (CKU) kuweza kuwasaidia wanafunzi katika chuo hiki.
Aliongeza na kusema kuwa ni jambo la kuigwa kwa tasisi nyingine lengo ni kuweza kusaidia vyuo mbalimbali hapa
nchini.