Ataitangaza Tanzania na vivutio vyake kwa wacheza sinema na walimbwende wengine wa
Marekani.
MCHEZA sinema na mlimbwende Deidre Lorenz kutoka katika jiji la New York nchini Marekani ameteuliwa kuwa balozi wa Mt. Kilimanjaro Marathon kwenye jiji hili la mapesa duniani la New York City (NYC).
Uteuzi huo ulifanywa kwa pamoja kati ya Rais wa Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 Mtanzania Onesmo Ngowi na mwanzilishi wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon Mmarekani Marie Frances hivi karibuni.
Uteuzi wa Lorenz ulizingatia uwezo wake wa kujichanganya katika makundi mbalimbali nchini Marekani hususan kundi la vijana matajiri. Hawa ndio wanaoweza kuwa watalii wenye uwezo wa kulipa pesa nyingi kwa huduma wanazopata watembeleapo vivutio mbalimbali vya kitalii nchini Tanzania.
Aidha, Lorenz anao uwezo wa kuunganisha wacheza sinema na walimbwene wengine na kuwashawishi kuja kutembelea vivutio mbalimbali hapa Tanzania. Deidre Lorenz alizaliwa katika jiji la Oregon na alianza kijihushisha na uchezaji wa vipindi watoto vya televisheni kabla ya kuhamia kwenye jiji la New York ambako alijiingiza kucheza filamu.
DeidreLorenz ameshacheza sinema nyingi kati ayke zikiwa zifuatazo: Santorini Blue, The Great Fight, Perfect Strangers na kuwahi kupata tuzo za: Tuzo ya Produza mpayailiyotolewa na Downtown Boca FilmFestival 2011 na kukabidhiwa na Stella Artois, tuzo ya chaguo la wadau wa sinema iliyotolewa na The NYC Downtown, tuzo ya TorontoIndependent iliyotolewa na Film Festival 2010. Mbali ya tuzo hizo Lorenz amewahi kupata tuzo mbalimbali za Oscar kama muingizaji bora.
Akitumia kampuni yake ya Thira Films LLC, Lorenz amekuwa anauza sinema zake kwenye miatandao mbalimbali. Hivi karubuni aliingia mkataba na kampuni ya Google kuuza kazi zake kwenye mtandao huu mkubwa duniani.
Kuteuliwa kwa Lorenz kunaipa Tanzania nafasi ya kujitangaza zaidi kwa kutumia mcheza sinema huyu maarufu duniani na hivyo kuipa nafasi kubwa nchi hii kujulikana zaidi kwa wacheza sinema ambao hupenda kutembelea maeneo ya kitalii.