DCB Bank Watambulisha DCB Jirani na DCB Mobile Sabasaba

Baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la DCB Commercial Bank kwenye maonesho ya kimataifa ya biashara maarufu kama SabaSaba wakipata maelezo juu ya huduma mbalimbali za DCB Commercial Bank.

Baadhi ya wananchi wakitembelea Banda la DCB Commercial Bank kwenye maonesho ya kimataifa ya biashara maarufu kama SabaSaba.

Baadhi ya wananchi wakitembelea Banda la DCB Commercial Bank kwenye maonesho ya kimataifa ya biashara maarufu kama SabaSaba.

Baadhi ya wafanyakazi wa DCB Commercial Bank wakitoa maelezo kwa wateja wa benki hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya biashara maarufu kama SabaSaba.

Baadhi ya wafanyakazi wa DCB Commercial Bank wakitoa maelezo kwa wateja wa benki hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya biashara maarufu kama SabaSaba.

DCB Commercial Bank imeendelea kuzitambulisha huduma zake mpya ikiwemo ya DCB Jirani ambayo inamuwezesha mteja wa banki hiyo kupata huduma za kibenki mahali popote kwa haraka na nafuu zaidi. Katika huduma ya DCB Jirani inamuwezesha mteja kuweka na kutoa pesa kwenye akaunti yake, kujua salio, kufungua akaunti na kupata taarifa fupi za akaunti, kutuma hela kutoka akaunti moja hadi nyingine, kununua muda wa maongezi wa simu, kupata huduma za M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money pamoja na kulipia huduma mbalimbali.

Kwa upande wa DCB Mobile ni huduma inayomuwezesha mteja wa benki hii kuendesha shughuli za kibenki kwa kutumia simu yake ya mkononi popote alipo. Kwa huduma ya DCB Mobile Mteja haitaji kwenda benki. Huduma hiyo inamuwezesha mteja kupokea pesa kutoka mitandao yote ya simu yenye huduma za kifedha, kutoa na kuweka fedha kwenye mitandao hiyo, Kutuma fedha kwenda akaunti nyingine na kuomba kitabu cha hudi na kuangalia salio.

Huduma zingine ni pamoja na kununua muda wa maongezi, kulipia huduma anuai kama vile Luku, Dawasco, DSTV, Startimes, TTCL, Uhuru One, NECTA na kupata huduma. Na pia mteja wa DCB Mobile anauwezo wa kubadilisha namba yake ya siri kwa kutumia simu popote alipo.

Huduma nyingine zinazotolewa na DCB Commercial Bank ni pamoja na DCB Connect, Western Union, Mkopo wa Numba, Mkopo wa Super SGL, Mkopo wa Biashara kwa watu Binafsi, Mkopo wa Vikundi, Mkopo kwa Wafanyakazi, Mikopo kwa Wafanyabiashara wadogo na wakati na huduma nyingine nyingi ya kifedha.