Mratibu wa Burudani wa Club mpya ya ‘Maisha Basement’ zamani New Club Maisha, Hemed Kavu (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Meneja wa Matukio, Robert Salehe na Kulia ni Meneja wa Burudani, Geofrey Gilla.
Meneja wa Burudani, Geofrey Gilla, akiwaonesha wanahabari ukumbi huo.
Meneja Mkuu wa Club hiyo, Allan Ngugi (kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo,Jean Claud Ciza wakati wa utambulisho wa uzinduzi huo kwa wanahabari.
Mtaalamu wa mitambo katika Clab hiyo, Mr Dong
akifanya vitu vyake.
Ukumbi huo unavyonekana kwa ndani.
Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Club mpya ya ‘Maisha Basement’. iliyopo katika Jengo la LAPF Towers lililopo mkabala na Makumbusho ya Taifa eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam
Hafla ya uzinduzi wa club hiyo zamani ikujulikana kama ‘New maisha Club’ utafanyika siku ya Idd Mosi katika ukumbi huo ambapo watu mbalimbali wamealikwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Mratibu wa Burudani wa Club hiyo, Hemed Kavu, alisema uzinduzi utafanyika kwa siku tatu tofauti ambazo ni leo, kesho na kilele ni siku siku hiyo ya Idd Mosi.
Alisema club hiyo mpya ambayo ni ya kisasa inauwezo wa kuchukua watu zaidi 700 kwa wakati mmoja na imejengwa katika kiwango cha kimataifa.
“Katika Siku hizi zote za uzinduzi kutakuwa na burudani mbalimbali…club yetu ina vifaa vya kisasa na dance floor ya kisasa yenye uwezo wa kurusha matukio moja kwa moja kama video na mechi na ina maegesho ya magari hivyo kuwa na ulinzi na usalama wa kutosha kwa mali za wateja” alisema.
Alisema hivi sasa wamekuja tofauti na walivyokuwa maisha club Masaki, kwani burudani zao zilikuwa zinaanza Jumatano mpaka Jumapili, lakini sasa zitaanza Jumatatu mpaka Jumatatu huku kiingilio kikiwa ni sh. 10,000 kwa siku zote.
Akitaja ratiba zao, alisema siku ya Jumatatu watakuwa na ‘Blue Monday nite’ kwa ajili ya wale wanaofanya kaz mwishoni mwa wiki, Jumanne ‘Meet and Greet nite’ huu ni usiku wa mashabiki kukutana na mastaa mbalimbali na Jumatano ni usiku wa Figisu figisu ambapo kutakuwa na burudani zote za Kiswahili.
“Alhamisi ni usiku wa ukae ambao tutakuwa tunapata burudani za bendi zetu za hapa nyumbani, Ijumaa ‘Winngle Nite’ usiku wa kupata ngoma za kisasa, RNB na East Africa Music, Jumamosi ‘Ibiza Nite’ kutakuwa na muziki wa kihindi na kiarabu, na Jumapili ‘Bongo Swagg’ ni usiku wa live performance kwa wanamuziki wetu,” alisema. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)