Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai katika lango la kuingilia katika shamba la Kilimo cha Kisasa la Mboga Mboga la Kilimanjaro Vegees Ltd lililopo Nshara Machame.
Mkuu wa wilaya ya Hai,akiwaongoza wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama ya wilaya Hai, pamoja na askari Mgambo wakiingia katika shamba la Kilimo cha Kisasa cha Mboga mboga la Kilimanjaro Vegees Ltd linalomilikiwa na Mbunge wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe.
Shamba la Kilimo cha Kisasa,(Green House) lililopo Nshara Machame wilaya ya Hai la Kilimanjaro Vegees Ltd.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai,wakiwa katika moja ya shamba hilo pamoja na asakari polisi wenye silaha wakiondoa miundo mbinu ya umwagiliaji pamoja na unyunyiziaji wa dawa .
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza katika eneo hilo wakati zoezi la kuondoa miundo mbinu katika eneo hilo ikiendelea.Zoezi hilo limefanyika kwa kile kinachodaiwa shughuli za kilimo kufanyika kando ya mto kinyume cha sharia.
Sehemu ya Shamba la Strawberry kabla ya kuondolewa miundo mbinu.
Askari Mgambo wakiondoa miundo mbinu ya umwailiaji katika shamba la Kilimoa cha Kisasa la Kilimanjaro Vegees Ltd linalomilikiwa na Mbunge wajimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Mipira maalumu iliyokuwa ikitumika katika umwagiliaji ikiwa imekatwa katwa .
Asakari Mgambo wakiendelea na zoezi la uondoshaji wa miundo mbinu.
Mkuu wa wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa akifuatilia zoezi la uondoshaji wa miundo mbinu ya umwagiliaji katika shamba hilo.
Mkuu wa wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akisaidia katika uondoshaji wa miondo mbinu katika shamba la kisasa la Kilimanjaro Vegees Ltd linalomilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Askari Mgambo wa kikata mipira kwa panga .
Zao la Strawberry ni moja wapo ya mazao yanyolimwa kisasa katika shmaba hilo.
Sehemu ya Mazao ambayo tayari yameanza kukomaa katika shamba hilo.
Kilimo cha kisasa cha zao la Nyanya pia kimekuwa kikifanyika katika shamba hilo.
Baadhi ya Green House zikiwa zimeondolewa wavu maalumu wa kuzuia wadudu kuingia ndani.
Na Dixon Busagaga wa Busagaga’s Orijino Blog.