TAARIFA zinasema dawa ya kuuwa magugu imegeuka shubiri baada ya kuanza kuua watu badala ya magugu kama ilivyokusudiwa. Shirika la Afya Duniani (WHO), linasema inaaminika kuwa dawa ya kuuwa magugu ndio chanzo cha vifo vya takribani watu 18 vilivyotokea Kusini-Magharibi mwa Nigeria, bila ya sababu kujulikana.
Hivi karibuni wakazi kadhaa wa Jimbo la Ondo walipoteza maisha muda mfupi baada ya kuhisi macho hayaoni sawasawa na kuumwa na vichwa kabla ya kuzimia. Wataalamu nwa WHO wanaamini kunauwezekano wakazi hao walifariki kwa kudhuriwa na dawa ya kuulia magugu.
Msemaji wa WHO alieleza kuwa uchunguzi wa awali uliofanywa hadi sasa kutafuta virusi au bacteria haukugundua kitu, hivyo kuamini kuwa upo uwezekano kwamba vifo hivyo vilisa-babishwa na dawa ya kuuwa magugu.
-BBC