SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa damu ya watu ambao wameugua ugonjwa wa Ebola na baadaye kupona inaweza kutumiwa kuwauguza wagonjwa wengine. Ufafanuzi huo umetolewa mjini Geneva na wataalam wa shirika hilo kabla ya kukubaliana kwamba hiyo ndio itakuwa njia ya haraka na salama dhidi ya ugonjwa wa Ebola.
Aidha wamesema sababu kuu ni kwamba imebainika kuwa kinga ya mwili katika damu ya mtu aliyepona inaweza kukabiliana na virusi hivyo na kuweza mnusuru. Wataalam hao pia wanataka matibabu mengine kuharakishwa ikiwemo dawa ya Zmapp pamoja na chanjo zengine mbili.
Idadi ya watu wanaodaiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Ebola imepita elfu mbili. Zaidi ya watu elfu nne wameambukizwa ugonjwa huo huku tiba yake ikiwa bado haijajulikana.
-BBC