
Binti Antu Mandoza akirudisha fomu za kuwania nafasi ya Ubunge Vijana Viti Maalumu kupitia CCM. Akihojiwa alisema amedhamiria kuinua maisha ya vijana kwa kuwatengenezea fursa na mbinu mbalimbali za kujiajiri, pia kutokukubali kutumika vibaya na makundi ya Kisiasa tunapoelekea Uchaguzi Mkuu kwani ni wajibu wetu ijana kuilinda amani yetu. Mgombea huyo pia ameeleza shauku yake kubwa ni kuwatumikia Vijana kwa kutatua changamoto ya Ajira na pia ametoa ahadi ya kushirikiana na Vijana bega kwa bega kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kagera.