CUF wamkabidhi JK mapendekezo yao juu ya Katiba Mpya

Rais Jakaya Kikwete amekutana na ujumbe a uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) Ikulu jijini Dar es Salaam na kuzungumza nao juu ya sheria ya kuanza mchakato wa kutafuta Katiba mpya. Ujumbe huo umeongozwa na Makama Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ally (kushoto) Rais Kikwete (kulia). (Picha na Ikulu)

Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa CUF na Serikali mara baada ya mazungumzo na CUF kukabidhi mapendekezo yao juu ya uundwaji Katiba Mpya.

Na Mwandishi Maalumu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na ujumbe wa serikali yake umekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Wananchi (CUF) ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Machano Khamis Ally kuhusu namna ya kuboresha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Mkutano huo umefanyika asubuhi ya Desemba 2, 2011, Ikulu, mjini Dar es Salaam na ujumbe wa CUF umemkabidhi Rais mapendekezo ya chama hicho kuhusu namna Sheria hiyo inavyoweza kuboreshwa.

Baada ya majadiliano ya saa mbili, pande hizo mbili zimekubaliana kujipa nafasi ya kutafakari zaidi na zitakutana tena jioni ya leo.