Akizungumza na baadhi ya wakurugenzi na mameneja wa benki hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya miaka 20 ya utendaji wa benki hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Charles Kimei alisema wamefanikiwa kuifanya taasisi hiyo kuwa kinara wa kutoa huduma bora. Alisema amana za wateja wa benki hiyo zimeongezeka zaidi ya mara 100 kutoka sh. bilioni 40 walizoanza nazo mwaka 1996 hadi sh. trilioni 4.2 iliyokuwepo Desemba 31 mwaka jana.
“Safari ya miaka 20 ilikuwa na misukosuko ikiwemo kupata hasara y ash. bilioni 1.8 mwaka 1997 lakini tunajivunia kusema tumepita salama na sasa tumekuwa taasisi bora ya fedha hapa Tanzania.
“Idadi ya bidhaa zetu, wateja na hata thamani ya benki pia imeongezeka… tunao waajiriwa 2,682 wenye nidhamu,” alisema Dk. Kimei huku akibainisha kwamba katika kampeni hizo watawekeza zaidi kwenye elimu. Alisema maadhimisho ya kuelekea kilele cha miaka 20 ya CRDB yatakayohitimishwa Juni mwaka huu yamepewa kauli mbiu ya ‘Benki inayokua na kuboresha maisha ya watu.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafitti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza kabla ya
kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sherehe za miaka 20 ya benki ya utendaji wa benki hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sherehe za miaka 20 ya benki ya utendaji wa benki hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo.
Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa beki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa beki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Dk. Charles Kimei (kushoto).
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB.