Baadhi ya wasanii na washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali.
Mmoja wa Wanasheria wa COSOTA, Maureen Fondo (kushoto) akiwaburudisha wanasemina kwa wimbo.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene akifungua semina hiyo ya COSOTA.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Haki Miliki kutoka Kenya (KECOBO), Marisela Ouma akiwasilisha mada katika semina hiyo.
Baadhi ya wasanii na washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA akizungumza katika semina hiyo.
Wasanii anuai wakijisajili kushiriki semina hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya COSOTA, akizungumza katika semina hiyo.
Msanii maharufu Bi. Natasha akizungumza jambo kwenye semina hiyo.
Msanii nguli Mzee Kitime naye aliongoza jopo la waendeshaji semina hiyo.
Wakili na Mhadhili kutoka kampuni ya Nex Law Advocates, Dr. Saudin Mwakaje akiwasilisha mada katika semina hiyo.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene akiserebuka baada ya kuvutiwa na moja ya burudani kwenye semina hiyo.
CHAMA cha Kusimamia Haki Miliki kwa Wasanii na Kazi za Sanaa (COSOTA) kimekutanisha wanachama wake na wadau wengine kisha kutoa semina juu ya namna bora ya kusimamia kazi zao ili ziwafaidishe zaidi kuliko wanavyofanya baadhi ya wasanii ambapo hujikuta kazi zao zinawanufaisha wengine.
Miongoni mwa mada ambazo zilitolewa kwa wanachama wa COSOTA pamoja na wadau mbalimbali ni namna ya kulinda haki za wasanii katika mazingira ya ulimwengu wa dijitali, namna sahihi ya kusimamia haki ya kazi za wasanii, ufafanuzi juu ya mikataba mbalimbali inayosimamia haki miliki pamoja na ulindaji wa haki miliki kwenye filamu.
Katika semina hiyo washiriki pia walielezwa juu ya umuhimu wa kusajili kazi zao na kampuni zinazosimamia kazi hizo pamoja na namna bora ya kuandaa mkataba kwa kuzingatia maslahi ya muhusika. Burudani mbalimbali zilitolewa katika semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Bi. Janeth Mbene.