KWELI kifo cha msanii maarufu Steven Kanumba zimewagusa wengi na si Tanzania pekee bali hata nje ya mipaka hiyo. Baadhi ya wasomaji wa Mtandao wa dev.kisakuzi.com kutoka nchini Congo DRC wametoa kilio chao kupitia kurasa ya maoni. Baadhi ya maoni yao ilikuwa kama ifuatavyo:-
“Mimi ni Hypolite BOMBORO kutoka Congo DRC/Bukavu mpendelevu marufu wa sinema ya Kanumba Steven ambaye leo anakuwa marehemu, nasikitika saaana na kifo ya musaani yule ambaye anatuacha na utamu ya kazi yake ambazo zilikuwa zinafurahisha walio wengi popote katika Bara letu la Afrika na ulimwenguni.
Na sema pole saana kwa familiya yake binafsi pamoja na kikundi chake ambapo alikuwa ndani, wasife moyo yaani ni Mungu ndiye hupanga kila kitu kabla duniya kuwekwa misingi yake na hakuna mtu anaye weza kuhepa hicho Mungu aliweka mbele yetu. Nafsi yake Mungu aipokeye katika ufalme wake,” ni maneno ya baadhi ya wasomaji kutoka Congo DRC.